Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 16 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿أَمۡ حَسِبۡتُمۡ أَن تُتۡرَكُواْ وَلَمَّا يَعۡلَمِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ جَٰهَدُواْ مِنكُمۡ وَلَمۡ يَتَّخِذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَا رَسُولِهِۦ وَلَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَلِيجَةٗۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ ﴾
[التوبَة: 16]
﴿أم حسبتم أن تتركوا ولما يعلم الله الذين جاهدوا منكم ولم يتخذوا﴾ [التوبَة: 16]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ni katika mipango ya Mwenyezi Mungu kuwajaribu waja Wake. Basi msidhani, enyi mkusanyiko wa Waumini, kwamba MwenyeziMungu Atawaacha bila ya mtihani ili Apate kuwajua, ujuzi uliyofunuka wazi kwa viumbe, waja Wake ambao wamemtakasia Mola wao katika jihadi yao na hawakuwafanya wasiokuwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Waumini kuwa ni washauri na marafiki. Na Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa vitendo vyenu vyote na Atawalipa kwa vitendo hivyo |