Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 31 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿ٱتَّخَذُوٓاْ أَحۡبَارَهُمۡ وَرُهۡبَٰنَهُمۡ أَرۡبَابٗا مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَٱلۡمَسِيحَ ٱبۡنَ مَرۡيَمَ وَمَآ أُمِرُوٓاْ إِلَّا لِيَعۡبُدُوٓاْ إِلَٰهٗا وَٰحِدٗاۖ لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ سُبۡحَٰنَهُۥ عَمَّا يُشۡرِكُونَ ﴾
[التوبَة: 31]
﴿اتخذوا أحبارهم ورهبانهم أربابا من دون الله والمسيح ابن مريم وما أمروا﴾ [التوبَة: 31]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mayahudi na Wanaswara wamewafanya wanavyuoni na watu wema kuwa ni waola wenye kuwaekea hukumu za sheria, wakawa wanajilazimisha kuzifuata na wanaacha sheria za Mwenyezi Mungu. Na pia walimfanya Al- Masīḥ, 'Īsā mwana wa Maryam, kuwa ni mungu, wakamuabudu. Na hakika Mwenyezi Mungu Amewaamrisha wao wamuabudu Yeye Peke Yake, bila ya mwingine. Yeye Ndiye Mungu wa haki. Hakuna mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Amejiepusha na Ametakasika na kila kile wanachokizua watu wa ushirikina na upotevu |