Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 32 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿يُرِيدُونَ أَن يُطۡفِـُٔواْ نُورَ ٱللَّهِ بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَيَأۡبَى ٱللَّهُ إِلَّآ أَن يُتِمَّ نُورَهُۥ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡكَٰفِرُونَ ﴾
[التوبَة: 32]
﴿يريدون أن يطفئوا نور الله بأفواههم ويأبى الله إلا أن يتم نوره﴾ [التوبَة: 32]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Makahfiri, kwa kukanusha kwao, wataka kuutangua Uislamu na kuzitangua hoja za Mwenyezi Mungu na dalili Zake, juu ya upweke Wake, Alizokuja nazo Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye. Na Mwenyezi Mungu Anakataa isipokuwa kuikamilisha dini Yake na kuipa nguvu, na kuliinua neno Lake, hata kama wenye kukanusha watalichukia hilo |