Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 48 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿لَقَدِ ٱبۡتَغَوُاْ ٱلۡفِتۡنَةَ مِن قَبۡلُ وَقَلَّبُواْ لَكَ ٱلۡأُمُورَ حَتَّىٰ جَآءَ ٱلۡحَقُّ وَظَهَرَ أَمۡرُ ٱللَّهِ وَهُمۡ كَٰرِهُونَ ﴾
[التوبَة: 48]
﴿لقد ابتغوا الفتنة من قبل وقلبوا لك الأمور حتى جاء الحق وظهر﴾ [التوبَة: 48]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Walipendelea wanafiki kuwafitini Waumini na Dini yao na kuwazuia wasiiifuate njia ya Mwenyezi Mungu kabla ya vita vya Tabūk, na mambo yao yakafunuka wakajulikana. Na walikuchafulia mambo, ewe Nabii, katika kuyavunja uliyokuja nayo, kama walivyofanya siku ya vita vya Uḥud na siku ya vita vya Khandaq. Na walikufanyia vitimbi mpaka usaidizi ukaja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Akawatia nguvu askari Wake na Akaipa ushindi dini Yake, pamoja na kuwa wao wanaichukia |