Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 70 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿أَلَمۡ يَأۡتِهِمۡ نَبَأُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ قَوۡمِ نُوحٖ وَعَادٖ وَثَمُودَ وَقَوۡمِ إِبۡرَٰهِيمَ وَأَصۡحَٰبِ مَدۡيَنَ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتِۚ أَتَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِۖ فَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظۡلِمَهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ ﴾
[التوبَة: 70]
﴿ألم يأتهم نبأ الذين من قبلهم قوم نوح وعاد وثمود وقوم إبراهيم﴾ [التوبَة: 70]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani haikuwajia wanafiki hawa habari ya wale waliopita, miongoni mwa watu wa Nūḥ, kabila la 'Ād, kabila la Thamūd, watu wa Ibrāhīm, watu wa Madyan na watu wa Lūṭ, walipowajia Mitume na wahyi na aya za Mwenyezi Mungu wakawakanusha? Wote hawa Mwenyezi Mungu Aliwateremshia adhabu Yake, kuwalipiza wao kwa matendo yao mabaya. Mwenyezi Mungu Hakuwa ni mwenye kuwadhulumu, lakini ni wao wenyewe walijidhulumu nafsi zao kwa kukanusha na kupinga |