Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 71 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۚ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَيُطِيعُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓۚ أُوْلَٰٓئِكَ سَيَرۡحَمُهُمُ ٱللَّهُۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ ﴾
[التوبَة: 71]
﴿والمؤمنون والمؤمنات بعضهم أولياء بعض يأمرون بالمعروف وينهون عن المنكر ويقيمون الصلاة﴾ [التوبَة: 71]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, waume na wake, wanasaidiana wao kwa wao, wanaamrisha watu kuamini na kufanya vitendo vyema na wanawakataza kukanusha na kufanya maasia, wanatekeleza Swala, wanatoa Zaka, wanamtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wanakomeka kufanya yale waliyokatazwa. Hao Mwenyezi Mungu Atawarehemu, Atawaokoa na adhabu Yake na Atawatia Peponi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwingi wa hekima katika sheria Zake na hukumu Zake |