Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 69 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿كَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ كَانُوٓاْ أَشَدَّ مِنكُمۡ قُوَّةٗ وَأَكۡثَرَ أَمۡوَٰلٗا وَأَوۡلَٰدٗا فَٱسۡتَمۡتَعُواْ بِخَلَٰقِهِمۡ فَٱسۡتَمۡتَعۡتُم بِخَلَٰقِكُمۡ كَمَا ٱسۡتَمۡتَعَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُم بِخَلَٰقِهِمۡ وَخُضۡتُمۡ كَٱلَّذِي خَاضُوٓاْۚ أُوْلَٰٓئِكَ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ ﴾
[التوبَة: 69]
﴿كالذين من قبلكم كانوا أشد منكم قوة وأكثر أموالا وأولادا فاستمتعوا بخلاقهم﴾ [التوبَة: 69]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika vitendo vyenu, enyi wanafiki, vya kucheza shere na ukafiri ni kama vitendo vya watu waliotangulia, waliokuwa na nguvu nyingi na mali na watoto zaidi kushinda nyinyi, wakajimakini na maisha ya kilimwengu, wakasterehe na vitu na ladha zilizomo. Basi na nyinyi, enyi wanafiki, mumestarehe kwa sehemu yenu ya matamanio yenye kumalizika kama starehe ya waliokuwa kabla yenu kwa mafungu yao ya vitu vya kilimwengu venye kumalizika. Na mumejiingiza katika kumzulia Mwenyezi Mungu urongo kama walivyojiingiza wale watu waliokuwa kabla yenu. Hao wenye kusifiwa kwa tabia hizi, ndio wale ambao mema yao yameondoka duniani na Akhera. Na wao ndio wenye kupata hasara kwa kuuza kwao sterehe za Akhera kwa vyeo na starehe za ulimwenguni |