×

Wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa hawakusema; nao wamekwisha sema neno la ukafiri, 9:74 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah At-Taubah ⮕ (9:74) ayat 74 in Swahili

9:74 Surah At-Taubah ayat 74 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 74 - التوبَة - Page - Juz 10

﴿يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ مَا قَالُواْ وَلَقَدۡ قَالُواْ كَلِمَةَ ٱلۡكُفۡرِ وَكَفَرُواْ بَعۡدَ إِسۡلَٰمِهِمۡ وَهَمُّواْ بِمَا لَمۡ يَنَالُواْۚ وَمَا نَقَمُوٓاْ إِلَّآ أَنۡ أَغۡنَىٰهُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ مِن فَضۡلِهِۦۚ فَإِن يَتُوبُواْ يَكُ خَيۡرٗا لَّهُمۡۖ وَإِن يَتَوَلَّوۡاْ يُعَذِّبۡهُمُ ٱللَّهُ عَذَابًا أَلِيمٗا فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَمَا لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٖ ﴾
[التوبَة: 74]

Wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa hawakusema; nao wamekwisha sema neno la ukafiri, na wakakufuru baada ya kusilimu kwao. Na wakajihimu kufanya ambayo hawakuweza kuyafikia. Na hawakuchukia ila kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake amewatajirisha kutokana na fadhila zake. Wakitubu itakuwa kheri kwao, na wakigeuka Mwenyezi Mungu atawaadhibu adhabu chungu duniani na Akhera. Na wala hawana katika ardhi mlinzi wala wa kuwanusuru

❮ Previous Next ❯

ترجمة: يحلفون بالله ما قالوا ولقد قالوا كلمة الكفر وكفروا بعد إسلامهم وهموا, باللغة السواحيلية

﴿يحلفون بالله ما قالوا ولقد قالوا كلمة الكفر وكفروا بعد إسلامهم وهموا﴾ [التوبَة: 74]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wanafiki wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba wao hawakusema kitu cha kumkosea Mtume na Waislamu. Wao ni warongo. Hakika wamesema neno la ukafiri na wametoka kwa hilo kwenye Uislamu, na wamejaribu kumdhuru Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, Mwenyezi Mungu hakuwawezesha kulifanya hilo. Na wanafiki hawakupata kitu chochote cha kumtia kombo na kumkosoa, isipokuwa ni kwamba Mwenyezi Mungu Aliwaneemesha akawapa utajiri kwa milango ya heri na baraka Aliyomfungulia Nabii Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye. Basi wakirudi makafiri hawa kwenye Imani na kutubia, hilo ni bora kwao, na wakigeuka nyuma au wakasalia hali ile walivyo, Mwenyezi Mungu Atawaadhibu adhabu iumizayo hapa duniani, kupitia mikono ya Waislamu, na kesho Akhera kwa Moto wa Jahanamu, na hapatakuwa na mwokoaji wa kuwaokoa wala msaidizi wa kuwakinga na janga la adhabu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek