Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 79 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿ٱلَّذِينَ يَلۡمِزُونَ ٱلۡمُطَّوِّعِينَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ فِي ٱلصَّدَقَٰتِ وَٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ إِلَّا جُهۡدَهُمۡ فَيَسۡخَرُونَ مِنۡهُمۡ سَخِرَ ٱللَّهُ مِنۡهُمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴾
[التوبَة: 79]
﴿الذين يلمزون المطوعين من المؤمنين في الصدقات والذين لا يجدون إلا جهدهم﴾ [التوبَة: 79]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na pamoja na ubahili wawanafiki, wale wanaotoa sadaka hawavuki salama na kero lao. Pindi wale matajiri wakitoa sadaka ya mali mengi, wanawatia kombo na kuwatuhumu kuwa wanajionesha. Na pindi mafukara wakitoa sadaka kulingana na uwezo wao, wanawafanyia shere na kusema kwa njia ya kuwachezea, «Sadaka yao hii itafalia nini?» Basi Mwenyezi Mungu Anawafanyia shere wanafiki hawa. Na wao watakuwa na adhabu kali iumizayo |