Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 81 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿فَرِحَ ٱلۡمُخَلَّفُونَ بِمَقۡعَدِهِمۡ خِلَٰفَ رَسُولِ ٱللَّهِ وَكَرِهُوٓاْ أَن يُجَٰهِدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَالُواْ لَا تَنفِرُواْ فِي ٱلۡحَرِّۗ قُلۡ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرّٗاۚ لَّوۡ كَانُواْ يَفۡقَهُونَ ﴾
[التوبَة: 81]
﴿فرح المخلفون بمقعدهم خلاف رسول الله وكرهوا أن يجاهدوا بأموالهم وأنفسهم في﴾ [التوبَة: 81]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Walifurahi wale waliojiweka nyuma wasimwandame Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani ziwashukiye, kwa kujikalia Madina wakienda kinyume na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na walichukia kupigana jihadi pamoja na Yeye kwa mali zao na nafsi Zao katika njia ya Mwenyezi Mungu na waliambiana wao kwa wao, «Msitoke katika kipindi cha joto.» Waambie, ewe Mtume, «Moto wa Jahanamu una joto zaidi,» lau wao wanalijua hilo |