The Quran in Swahili - Surah Abasa translated into Swahili, Surah Abasa in Swahili. We provide accurate translation of Surah Abasa in Swahili - السواحيلية, Verses 42 - Surah Number 80 - Page 585.

| عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ (1) Alikunja kipaji na akageuka |
| أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ (2) Kwa sababu alimjia kipofu |
| وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ (3) Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika |
| أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ (4) Au atawaidhika, na mawaidha yamfae |
| أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ (5) Ama ajionaye hana haja |
| فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ (6) Wewe ndio unamshughulikia |
| وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ (7) Na si juu yako kama hakutakasika |
| وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ (8) Ama anaye kujia kwa juhudi |
| وَهُوَ يَخْشَىٰ (9) Naye anaogopa |
| فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ (10) Ndio wewe unampuuza |
| كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ (11) Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana |
| فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ (12) Basi anaye penda akumbuke |
| فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ (13) Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa |
| مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ (14) Zilizo inuliwa, zilizo takaswa |
| بِأَيْدِي سَفَرَةٍ (15) Zimo mikononi mwa Malaika waandishi |
| كِرَامٍ بَرَرَةٍ (16) Watukufu, wema |
| قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ (17) Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha |
| مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ (18) Kwa kitu gani amemuumba |
| مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ (19) Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria |
| ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ (20) Kisha akamsahilishia njia |
| ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ (21) Kisha akamfisha, akamtia kaburini |
| ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ (22) Kisha apendapo atamfufua |
| كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ (23) La! Hajamaliza aliyo muamuru |
| فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ (24) Hebu mtu na atazame chakula chake |
| أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا (25) Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu |
| ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا (26) Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu |
| فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا (27) Kisha tukaotesha humo nafaka |
| وَعِنَبًا وَقَضْبًا (28) Na zabibu, na mimea ya majani |
| وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا (29) Na mizaituni, na mitende |
| وَحَدَائِقَ غُلْبًا (30) Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara |
| وَفَاكِهَةً وَأَبًّا (31) Na matunda, na malisho ya wanyama |
| مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ (32) Kwa manufaa yenu na mifugo yenu |
| فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ (33) Basi utakapo kuja ukelele |
| يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ (34) Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye |
| وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ (35) Na mamaye na babaye |
| وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ (36) Na mkewe na wanawe |
| لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ (37) Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha |
| وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ (38) Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri |
| ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ (39) Zitacheka, zitachangamka |
| وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ (40) Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi |
| تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ (41) Giza totoro litazifunika |
| أُولَٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ (42) Hao ndio makafiri watenda maovu |