القرآن باللغة السواحيلية - سورة عبس مترجمة إلى اللغة السواحيلية، Surah Abasa in Swahili. نوفر ترجمة دقيقة سورة عبس باللغة السواحيلية - Swahili, الآيات 42 - رقم السورة 80 - الصفحة 585.
عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ (1) Alikunja kipaji na akageuka |
أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ (2) Kwa sababu alimjia kipofu |
وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ (3) Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika |
أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ (4) Au atawaidhika, na mawaidha yamfae |
أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ (5) Ama ajionaye hana haja |
فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ (6) Wewe ndio unamshughulikia |
وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ (7) Na si juu yako kama hakutakasika |
وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ (8) Ama anaye kujia kwa juhudi |
وَهُوَ يَخْشَىٰ (9) Naye anaogopa |
فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ (10) Ndio wewe unampuuza |
كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ (11) Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana |
فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ (12) Basi anaye penda akumbuke |
فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ (13) Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa |
مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ (14) Zilizo inuliwa, zilizo takaswa |
بِأَيْدِي سَفَرَةٍ (15) Zimo mikononi mwa Malaika waandishi |
كِرَامٍ بَرَرَةٍ (16) Watukufu, wema |
قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ (17) Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha |
مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ (18) Kwa kitu gani amemuumba |
مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ (19) Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria |
ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ (20) Kisha akamsahilishia njia |
ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ (21) Kisha akamfisha, akamtia kaburini |
ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ (22) Kisha apendapo atamfufua |
كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ (23) La! Hajamaliza aliyo muamuru |
فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ (24) Hebu mtu na atazame chakula chake |
أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا (25) Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu |
ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا (26) Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu |
فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا (27) Kisha tukaotesha humo nafaka |
وَعِنَبًا وَقَضْبًا (28) Na zabibu, na mimea ya majani |
وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا (29) Na mizaituni, na mitende |
وَحَدَائِقَ غُلْبًا (30) Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara |
وَفَاكِهَةً وَأَبًّا (31) Na matunda, na malisho ya wanyama |
مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ (32) Kwa manufaa yenu na mifugo yenu |
فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ (33) Basi utakapo kuja ukelele |
يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ (34) Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye |
وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ (35) Na mamaye na babaye |
وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ (36) Na mkewe na wanawe |
لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ (37) Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha |
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ (38) Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri |
ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ (39) Zitacheka, zitachangamka |
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ (40) Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi |
تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ (41) Giza totoro litazifunika |
أُولَٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ (42) Hao ndio makafiri watenda maovu |