إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ (1) Mbingu itapo chanika |
وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ (2) Na nyota zitapo tawanyika |
وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ (3) Na bahari zitakapo pasuliwa |
وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ (4) Na makaburi yatapo fukuliwa |
عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ (5) Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma |
يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ (6) Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu |
الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ (7) Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha |
فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاءَ رَكَّبَكَ (8) Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga |
كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ (9) Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo |
وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ (10) Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu |
كِرَامًا كَاتِبِينَ (11) Waandishi wenye hishima |
يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ (12) Wanayajua mnayo yatenda |
إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ (13) Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema |
وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ (14) Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni |
يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ (15) Wataingia humo Siku ya Malipo |
وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ (16) Na hawatoacha kuwamo humo |
وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ (17) Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani |
ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ (18) Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani |
يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْئًا ۖ وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّهِ (19) Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu |