| إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ (1) Mbingu itapo chanika
 | 
| وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ (2) Na nyota zitapo tawanyika
 | 
| وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ (3) Na bahari zitakapo pasuliwa
 | 
| وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ (4) Na makaburi yatapo fukuliwa
 | 
| عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ (5) Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma
 | 
| يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ (6) Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu
 | 
| الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ (7) Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha
 | 
| فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاءَ رَكَّبَكَ (8) Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga
 | 
| كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ (9) Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo
 | 
| وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ (10) Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu
 | 
| كِرَامًا كَاتِبِينَ (11) Waandishi wenye hishima
 | 
| يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ (12) Wanayajua mnayo yatenda
 | 
| إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ (13) Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema
 | 
| وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ (14) Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni
 | 
| يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ (15) Wataingia humo Siku ya Malipo
 | 
| وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ (16) Na hawatoacha kuwamo humo
 | 
| وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ (17) Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani
 | 
| ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ (18) Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani
 | 
| يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْئًا ۖ وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّهِ (19) Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu
 |