Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 104 - يُونس - Page - Juz 11
﴿قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِن كُنتُمۡ فِي شَكّٖ مِّن دِينِي فَلَآ أَعۡبُدُ ٱلَّذِينَ تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِنۡ أَعۡبُدُ ٱللَّهَ ٱلَّذِي يَتَوَفَّىٰكُمۡۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ﴾
[يُونس: 104]
﴿قل ياأيها الناس إن كنتم في شك من ديني فلا أعبد الذين﴾ [يُونس: 104]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu hawa, «Iwapo muko kwenye shaka juu ya usawa wa Dini yangu ambayo nimewaitia kwayo, nayo ni Uislamu, na juu ya uthabiti wangu na kujikita kwangu juu yake, pamoja ya kuwa nyinyi muna matumaini ya kuniepusha nayo, basi mimi sitamuabudu katika hali yoyote ile, yoyote miongoni mwa wale mnaowaabudu mkajifanyia masanamu na mizimu, lakini namuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Mwenye kuwafisha na kuzitwaa roho zenu, na nimeamrishwa niwe ni miongoni mwa wenye kumuamini na wenye kufuata Sheria Zake kivitendo.» |