×

Nao, badala ya Mwenyezi Mungu, wanaabudu wasio wadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema: 10:18 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Yunus ⮕ (10:18) ayat 18 in Swahili

10:18 Surah Yunus ayat 18 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 18 - يُونس - Page - Juz 11

﴿وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُمۡ وَلَا يَنفَعُهُمۡ وَيَقُولُونَ هَٰٓؤُلَآءِ شُفَعَٰٓؤُنَا عِندَ ٱللَّهِۚ قُلۡ أَتُنَبِّـُٔونَ ٱللَّهَ بِمَا لَا يَعۡلَمُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ ﴾
[يُونس: 18]

Nao, badala ya Mwenyezi Mungu, wanaabudu wasio wadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema: Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu! Sema: Je! Mnamwambia Mwenyezi Mungu asiyo yajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Subhanahu wa Taa'la! Ametakasika na ametukuka na hao wanao mshirikisha naye

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ويعبدون من دون الله ما لا يضرهم ولا ينفعهم ويقولون هؤلاء شفعاؤنا, باللغة السواحيلية

﴿ويعبدون من دون الله ما لا يضرهم ولا ينفعهم ويقولون هؤلاء شفعاؤنا﴾ [يُونس: 18]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na hawa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu na asiyekuwa Yeye wanaviabudu visivyowadhuru chochote wala kuwanufaisha ulimwenguni wala Akhera, na wanasema, «Sisi tunawaabudu wao ili watuombee mbele ya Mwenyezi Mungu.» Waambie, ewe Mtume, «Je, mnampa habari Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, jambo Asilolijua, katika mbingu au katika ardhi, kuhusu mambo ya waombezi hawa?» Kwa hakika lau kulikuwa na waombezi katika hizo wa kuwaombea nyinyi mbele Yake, Angalikuwa na ujuzi zaidi kuhusu wao kuliko nyinyi.» Kwani Mwenyenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameepukana na wanachokifanya washirikina hawa cha kushirikisha kwao, katika ibada Yake, vitu visivyodhuru wala kunufaisha
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek