×

Sema: Je! Yupo katika miungu yenu ya ushirikina aliye anzisha kuumba viumbe, 10:34 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Yunus ⮕ (10:34) ayat 34 in Swahili

10:34 Surah Yunus ayat 34 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 34 - يُونس - Page - Juz 11

﴿قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۚ قُلِ ٱللَّهُ يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ ﴾
[يُونس: 34]

Sema: Je! Yupo katika miungu yenu ya ushirikina aliye anzisha kuumba viumbe, na kisha akavirejesha? Huwaje, basi, mkadanganywa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: قل هل من شركائكم من يبدأ الخلق ثم يعيده قل الله يبدأ, باللغة السواحيلية

﴿قل هل من شركائكم من يبدأ الخلق ثم يعيده قل الله يبدأ﴾ [يُونس: 34]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Je, kuna yoyote, miongoni mwa waungu wenu na waabudiwa wenu, mwenye kuanzisha kuumba chochote kisicho na asili (ya mfano uliotangulia) kisha akifanye kitoweke baada ya kukianzisha, kisha akirudishe kama namna kilivyokuwa kabla hajakifanya kitoweke?» Kwa hakika, wao hawawezi kufanya madai hayo. Sema, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Anayeanzisha kuumba kisha Akakifanya kitoweke kile Alichokiumba, kisha Akakirudisha. Basi ni vipi nyinyi mnajiepusha na njia ya haki na kufuata ubatilifu, nao ni kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu?»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek