Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 5 - يُونس - Page - Juz 11
﴿هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ ٱلشَّمۡسَ ضِيَآءٗ وَٱلۡقَمَرَ نُورٗا وَقَدَّرَهُۥ مَنَازِلَ لِتَعۡلَمُواْ عَدَدَ ٱلسِّنِينَ وَٱلۡحِسَابَۚ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۚ يُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ ﴾
[يُونس: 5]
﴿هو الذي جعل الشمس ضياء والقمر نورا وقدره منازل لتعلموا عدد السنين﴾ [يُونس: 5]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Ndiye ambaye Alilifanya jua kuwa d,iyā’ (mwangaza), Akaufanya mwezi kuwa ni nūr (mng’aro) na Akaupangia mwezi njia zake za kupita. Ikawa kwa jua zinajulikana siku, na kwa mwezi inajulikana miezi na miaka. Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Hakuumba jua na mwezi isipokuwa ni hekima kubwa, na kuonesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu na ujuzi Wake; Anafafanua hoja na dalili kwa watu wanaojua hekima ya utengenezaji wa uumbaji |