Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 43 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَمِنۡهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيۡكَۚ أَفَأَنتَ تَهۡدِي ٱلۡعُمۡيَ وَلَوۡ كَانُواْ لَا يُبۡصِرُونَ ﴾
[يُونس: 43]
﴿ومنهم من ينظر إليك أفأنت تهدي العمي ولو كانوا لا يبصرون﴾ [يُونس: 43]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwao kuna wanaokutazama wewe na dalili za unabii wako wa kweli, lakini wao hawaioni nuru ya Imani Aliyokupa Mwenyezi Mungu. Je, unaweza , ewe Mtume, kuwaumbia vipofu macho ya kuwafanya wao waongoke. Vilevile huwezi kuwaongoa wao iwapo hawana busara. Hakika yote hayo yako kwa Mwenyezi Mungu |