Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 46 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعۡضَ ٱلَّذِي نَعِدُهُمۡ أَوۡ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيۡنَا مَرۡجِعُهُمۡ ثُمَّ ٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ ﴾
[يُونس: 46]
﴿وإما نرينك بعض الذي نعدهم أو نتوفينك فإلينا مرجعهم ثم الله شهيد﴾ [يُونس: 46]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na iwapo tutakuonesha, ewe Mtume, katika uhai wako baadhi ya mateso tunayowaahidi duniani, au tukakufisha kabla hatujakuonesha hayo kwao, ni kwetu sisi peke yetu marejeo ya mambo yao katika hali zote mbili, kisha Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa vitendo vyao waliokuwa wakivifanya duniani, hakuna chochote kati ya hivyo kinafichika Kwake, na Atawalipa malipo yao wanayostahiki kwa vitendo vyao hivyo |