Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 47 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَلِكُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولٞۖ فَإِذَا جَآءَ رَسُولُهُمۡ قُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ ﴾
[يُونس: 47]
﴿ولكل أمة رسول فإذا جاء رسولهم قضي بينهم بالقسط وهم لا يظلمون﴾ [يُونس: 47]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kila ummah uliopita kabla yenu, enyti watu, ulikuwa na mjumbe niliyemtuma kwao, kama nilivyomtuma Muhammad kwenu Alinganie kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu na kuwa na utiifu Kwake. Basi huyo mjumbe wao atakapokuja Akhera, hapo kutaamuliwa baina yao kwa uadilifu, na wao hawatadhulumiwa katika malipo ya matendo yao chochote |