Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 57 - يُونس - Page - Juz 11
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَتۡكُم مَّوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَشِفَآءٞ لِّمَا فِي ٱلصُّدُورِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ ﴾
[يُونس: 57]
﴿ياأيها الناس قد جاءتكم موعظة من ربكم وشفاء لما في الصدور وهدى﴾ [يُونس: 57]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi watu yamewajia nyinyi mawaidha kutoka kwa Mola wenu yanayowakumbusha mateso ya Mwenyezi Mungu na yanayowaonya makamio Yake, nayo ni Qur’ani na yale iliyoyakusanya ya miujiza na mawaidha ili kuzitengeneza tabia zenu na matendo yenu. Na ndani yake muna dawa ya yaliyomo nyoyoni ya ujinga na ushirikina na magonjwa mengineyo, na muna uongofu kwa viumbe wenye kuifuata iwaokoe na maangamivu. Mwanyezi mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Ameijaalia ni neema na rehema kwa Waumini. Na Amewahusu Waumini kwa hilo, kwa kuwa wao ndio wenye kunufaika na Imani. Ama makafiri, hiyo Qur’ani kwao ni giza |