Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 58 - يُونس - Page - Juz 11
﴿قُلۡ بِفَضۡلِ ٱللَّهِ وَبِرَحۡمَتِهِۦ فَبِذَٰلِكَ فَلۡيَفۡرَحُواْ هُوَ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ ﴾
[يُونس: 58]
﴿قل بفضل الله وبرحمته فبذلك فليفرحوا هو خير مما يجمعون﴾ [يُونس: 58]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu wote, «Kwa wema wa Mwenyezi Mungu na rehema Yake, basi na wawe na furaha.» Wema wa Mwenyezi mungu na rehema Yake ni Uislamu ambao ni uongofu na ni Dini ya haki aliyokuja nayo Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwani Uislamu ambao Mwenyezi Mungu Amewaita wao waufuate, na Qur’ani ambayo Aliiteremsha kwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye ni bora kuliko taka za ulimwengu wanazozikusanya na anasa zilizomo ndani yake zenye kutoeka kuondoka |