Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 90 - يُونس - Page - Juz 11
﴿۞ وَجَٰوَزۡنَا بِبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱلۡبَحۡرَ فَأَتۡبَعَهُمۡ فِرۡعَوۡنُ وَجُنُودُهُۥ بَغۡيٗا وَعَدۡوًاۖ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَدۡرَكَهُ ٱلۡغَرَقُ قَالَ ءَامَنتُ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱلَّذِيٓ ءَامَنَتۡ بِهِۦ بَنُوٓاْ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَأَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ ﴾
[يُونس: 90]
﴿وجاوزنا ببني إسرائيل البحر فأتبعهم فرعون وجنوده بغيا وعدوا حتى إذا أدركه﴾ [يُونس: 90]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tuliwakatia bahari Wana wa Isrāīl mpaka wakaivuka, wakafuatwa na Fir'awn na askari wake, kwa udhalimu na uadui, wakafuata njia ya bahari nyuma yao, mpaka Fir'awn alipozungukwa na hali ya kuzama alisema kwamba hapana Mola isipokuwa yule ambaye Wana wa Isrāī wamemuamini, na mimi ni miongoni mwa wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu wenye kujisalimisha Kwake kwa kufuata na kutii |