Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 102 - هُود - Page - Juz 12
﴿وَكَذَٰلِكَ أَخۡذُ رَبِّكَ إِذَآ أَخَذَ ٱلۡقُرَىٰ وَهِيَ ظَٰلِمَةٌۚ إِنَّ أَخۡذَهُۥٓ أَلِيمٞ شَدِيدٌ ﴾
[هُود: 102]
﴿وكذلك أخذ ربك إذا أخذ القرى وهي ظالمة إن أخذه أليم شديد﴾ [هُود: 102]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kama nilivyowapatiliza kwa adhabu watu wa miji iliyodhulumu kwa kuenda kinyume na amri yangu na kuwakanusha Mitume wangu, nitawapatiliza wengineo miongoni mwa watu wa miji wakizidhulumu nafsi zao kwa kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumuasi Yeye na kuwakanusha Mitume Wake. Hakika mapatilizo Yake ya mateso ni makali, yenye kuumiza, yaliyo magumu |