Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 114 - هُود - Page - Juz 12
﴿وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَيِ ٱلنَّهَارِ وَزُلَفٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِۚ إِنَّ ٱلۡحَسَنَٰتِ يُذۡهِبۡنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ ذَٰلِكَ ذِكۡرَىٰ لِلذَّٰكِرِينَ ﴾
[هُود: 114]
﴿وأقم الصلاة طرفي النهار وزلفا من الليل إن الحسنات يذهبن السيئات ذلك﴾ [هُود: 114]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tekeleza Swala, ewe Nabii, kwa njia ya ukamilifu katika ncha mbili za mchana: asubuhi na jioni, na katika nyakati za usiku. Kwani kufanya mema kunafuta dhambi zilizopita na kuondoa athari zake. Kuamrisha kusimamisha Swala na kueleza kwamba mema huondoa mabaya ni mawaidha kwa anayewaidhika nayo na akakumbuka |