Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 29 - هُود - Page - Juz 12
﴿وَيَٰقَوۡمِ لَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مَالًاۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۚ وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْۚ إِنَّهُم مُّلَٰقُواْ رَبِّهِمۡ وَلَٰكِنِّيٓ أَرَىٰكُمۡ قَوۡمٗا تَجۡهَلُونَ ﴾
[هُود: 29]
﴿وياقوم لا أسألكم عليه مالا إن أجري إلا على الله وما أنا﴾ [هُود: 29]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Nūḥ, amani imshukiye, akaendelea kuwaambia watu wake, «Enyi watu wangu, siwaombi kwa kuwaita nyinyi kumpwekesha Mwenyezi Mungu, munipatie mali baada ya kuamini kwenu, kwani malipo ya ushauri wangu kwenu yako kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na si shughuli yangu mimi kuwafukuza Waumini, kwani wao ni wenye kukutana na Mola wao Siku ya Kiyama. Lakini mimi nawaona nyinyi kuwa ni watu msiojua, kwa kuwa mnaniamrisha niwafukuze vipenzi vya Mwenyezi Mungu na niwaepushe na mimi |