Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 31 - هُود - Page - Juz 12
﴿وَلَآ أَقُولُ لَكُمۡ عِندِي خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ وَلَآ أَقُولُ إِنِّي مَلَكٞ وَلَآ أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزۡدَرِيٓ أَعۡيُنُكُمۡ لَن يُؤۡتِيَهُمُ ٱللَّهُ خَيۡرًاۖ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا فِيٓ أَنفُسِهِمۡ إِنِّيٓ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[هُود: 31]
﴿ولا أقول لكم عندي خزائن الله ولا أعلم الغيب ولا أقول إني﴾ [هُود: 31]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Na wala siwaambii nyinyi kuwa mimi nina mahazina ya Mwenyezi Mungu, wala mimi siyajui yasiyoonekana, na mimi si mmoja kati ya Malaika, wala siwaambii hawa mnaowadharau miongoni mwa madhaifu wa Waumini kwamba Mwenyezi Mungu hatawapa malipo mema ya matendo yao. Mwenyezi Mungu, Peke Yake, ni Mjuzi kabisa kwa yaliyomo ndani ya vifua vyao na nyoyo zao. Na nikifanya hivyo, basi mimi wakati huo nitakuwa ni miongoni mwa wale wenye kujidhulumu wao wenyewe na kuwadhulumu wengineo» |