Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 40 - هُود - Page - Juz 12
﴿حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَمۡرُنَا وَفَارَ ٱلتَّنُّورُ قُلۡنَا ٱحۡمِلۡ فِيهَا مِن كُلّٖ زَوۡجَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِ وَأَهۡلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيۡهِ ٱلۡقَوۡلُ وَمَنۡ ءَامَنَۚ وَمَآ ءَامَنَ مَعَهُۥٓ إِلَّا قَلِيلٞ ﴾
[هُود: 40]
﴿حتى إذا جاء أمرنا وفار التنور قلنا احمل فيها من كل زوجين﴾ [هُود: 40]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mpaka ilipokuja amri yetu ya kuwaangamiza wao kama tulivyomuahidi Nūḥ, kwa hilo, na maji yakachimbuka kwa nguvu kutoka kwenye tanuri, mahala pa kuchomea mikate, ikiwa ni alama ya kuja adhabu, tulimuambia Nūḥ, «Beba ndani ya jahazi kila aina, miongoni mwa aina za wanyama wa kiume na wa kike, na uwabebe ndani yake watu wa nyumbani kwako, isipokuwa yule aliyetanguliwa na Neno kuwa wataadhibiwa katika wale wasiomuamini Mwenyezi Mungu kama mtoto wake na mke wake, na ubebe ndani yake aliyeamini pamoja na wewe katika watu wako.» Na hakuna aliyeamini pamoja na yeye isipokuwa wachache ingawa yeye alikaa na wao kwa muda mrefu |