Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 41 - هُود - Page - Juz 12
﴿۞ وَقَالَ ٱرۡكَبُواْ فِيهَا بِسۡمِ ٱللَّهِ مَجۡر۪ىٰهَا وَمُرۡسَىٰهَآۚ إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ ﴾
[هُود: 41]
﴿وقال اركبوا فيها بسم الله مجراها ومرساها إن ربي لغفور رحيم﴾ [هُود: 41]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Nūḥ alisema kuwaambia walioamini pamoja na yeye, «Pandeni kwenye jahazi kwa jina la Mwenyezi Mungu. Kwa jina la Mwenyezi Mungu itatembea majini, na kwa jina la Mwenyezi Mungu itafika mwisho wa kwenda kwake na kutia nanga kwake. Hakika Mola wangu ni Mwingi wa kusamehe dhambi za mwenye kutubia na kurudi Kwake miongoni mwa waja Wake, ni Mwingi wa huruma kwao kwa kutowaadhibu baada ya kutubia |