Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 66 - هُود - Page - Juz 12
﴿فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا صَٰلِحٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَمِنۡ خِزۡيِ يَوۡمِئِذٍۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡقَوِيُّ ٱلۡعَزِيزُ ﴾
[هُود: 66]
﴿فلما جاء أمرنا نجينا صالحا والذين آمنوا معه برحمة منا ومن خزي﴾ [هُود: 66]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi amri yetu ilipokuja ya kuwaangamiza Thamūd, tulimuokoa Ṣāliḥ na walioamini pamoja na yeye na maangamivu kwa rehema kutoka kwetu. Na tuliwaokoa wao na unyonge wa Siku hiyo na udhalilifu wake. Hakika Mola wako, ewe Mtume, Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye ushindi. Na miongoni mwa nguvu Zake na ushindi Wake ni kuwa Aliwaangamiza watu wenye kupita kiasi kwenye uasi na akawaokoa Mitume na wafuasi wao |