Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 7 - هُود - Page - Juz 12
﴿وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ وَكَانَ عَرۡشُهُۥ عَلَى ٱلۡمَآءِ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلٗاۗ وَلَئِن قُلۡتَ إِنَّكُم مَّبۡعُوثُونَ مِنۢ بَعۡدِ ٱلۡمَوۡتِ لَيَقُولَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ ﴾
[هُود: 7]
﴿وهو الذي خلق السموات والأرض في ستة أيام وكان عرشه على الماء﴾ [هُود: 7]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Yeye Ndiye Ambaye Aliumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake kwa Siku Sita na Arshi Yake ilikuwa iko juu ya maji kabla ya hapo, Apate kuwajaribu nyinyi, ni nani kati yenu mzuri zaidi wa utiifu na utendaji. Utendaji wenye kumtakasia Mwenyezi Mungu, wenye kulingana na vile Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, alivyokuwa. Na lau unasema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina wa watu wako, «Nyinyi mtafufuliwa mkiwa hai baada ya kufa kwenu.» Watafanya haraka kukanusha na watasema, «Haikuwa hii Qur’ani unayotusomea isipokuwa ni uchawi ulio wazi.» |