Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 8 - هُود - Page - Juz 12
﴿وَلَئِنۡ أَخَّرۡنَا عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابَ إِلَىٰٓ أُمَّةٖ مَّعۡدُودَةٖ لَّيَقُولُنَّ مَا يَحۡبِسُهُۥٓۗ أَلَا يَوۡمَ يَأۡتِيهِمۡ لَيۡسَ مَصۡرُوفًا عَنۡهُمۡ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ ﴾
[هُود: 8]
﴿ولئن أخرنا عنهم العذاب إلى أمة معدودة ليقولن ما يحبسه ألا يوم﴾ [هُود: 8]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau tutawacheleweshea adhabu, hawa washirikina, mpaka muda maalumu, wakaona imekawia, watasema kwa njia ya shere na kukanusha, «Ni kitu gani kinachozuia adhabu hii isitukie ikiwa ni kweli?» Jueni mtanabahi, siku itakapowajia adhabu hiyo hakuna atakayeweza kuwaondolea, wala yoyote mwenye kuizuia, na iatawazunguka wao, kutoka kila upande, adhabu waliokuwa wakiifanyia shere kabla haijawajia |