Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 86 - هُود - Page - Juz 12
﴿بَقِيَّتُ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِحَفِيظٖ ﴾
[هُود: 86]
﴿بقية الله خير لكم إن كنتم مؤمنين وما أنا عليكم بحفيظ﴾ [هُود: 86]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Kile kitakachosalia kwenu cha faida ya halali, baada ya kutimiza vipimo na mizani, kina baraka na ni chema kwenu kuliko kile mkichukuacho cha pato la haramu kwa njia ya kupunja na mfano wake. Iwapo nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu kikweli, basi fuateni amri Yake. Na mimi si mtunzi kwenu wa kuwahesabia matendo yenu.» |