Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 19 - يُوسُف - Page - Juz 12
﴿وَجَآءَتۡ سَيَّارَةٞ فَأَرۡسَلُواْ وَارِدَهُمۡ فَأَدۡلَىٰ دَلۡوَهُۥۖ قَالَ يَٰبُشۡرَىٰ هَٰذَا غُلَٰمٞۚ وَأَسَرُّوهُ بِضَٰعَةٗۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ ﴾
[يُوسُف: 19]
﴿وجاءت سيارة فأرسلوا واردهم فأدلى دلوه قال يابشرى هذا غلام وأسروه بضاعة﴾ [يُوسُف: 19]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Likaja kundi la wasafiri wakamtuma mwenye kuwatafutia maji, alipoiteremsha ndoo yake kisimani, Yūsuf aliishikilia. Hapo mchota maji alifurahi na akachangamka kwa kumuokota mtoto na akasema, «Ni bishara njema iliyoje! Huyu ni mtoto wa kiume mzuri.» Mchota maji na wenzake walimficha Yūsuf asijulikane na wasafiri wengine wasiwaoneshe, na wakasema, «Hii ni bidhaa tuumeinunua.» Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi mno wa wanayomfanyia Yūsuf |