Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 18 - يُوسُف - Page - Juz 12
﴿وَجَآءُو عَلَىٰ قَمِيصِهِۦ بِدَمٖ كَذِبٖۚ قَالَ بَلۡ سَوَّلَتۡ لَكُمۡ أَنفُسُكُمۡ أَمۡرٗاۖ فَصَبۡرٞ جَمِيلٞۖ وَٱللَّهُ ٱلۡمُسۡتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ ﴾
[يُوسُف: 18]
﴿وجاءوا على قميصه بدم كذب قال بل سولت لكم أنفسكم أمرا فصبر﴾ [يُوسُف: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wakaja na kanzu yake ikiwa imerowa kwa damu ambayo si ya Yūsuf, ili iwe ni ushahidi juu ya ukweli wao, ikawa ni dalili ya urongo wao, kwa kuwa kanzu haikuchanika. Baba yao Ya’qūb, amani imshukiye, akawaaambia, «Mambo sivyo kama mlivyosema, bali ni nafsi zenu zenye kuamrisha uovu ziliwapambia jambo ovu kumfanyia Yūsuf, mkaliona ni zuri na mkalifanya. Basi nitasubiri subira nzuri isiyokuwa na malalamishi kwa kiumbe chochote, na namuomba Mwenyezi Mungu msaada wa kuweza kuubeba huo urongo mnaoupanga; sitegemei uwezo wangu wala nguvu zangu |