Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 23 - يُوسُف - Page - Juz 12
﴿وَرَٰوَدَتۡهُ ٱلَّتِي هُوَ فِي بَيۡتِهَا عَن نَّفۡسِهِۦ وَغَلَّقَتِ ٱلۡأَبۡوَٰبَ وَقَالَتۡ هَيۡتَ لَكَۚ قَالَ مَعَاذَ ٱللَّهِۖ إِنَّهُۥ رَبِّيٓ أَحۡسَنَ مَثۡوَايَۖ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّٰلِمُونَ ﴾
[يُوسُف: 23]
﴿وراودته التي هو في بيتها عن نفسه وغلقت الأبواب وقالت هيت لك﴾ [يُوسُف: 23]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mke wa yule kiongozi, ambaye Yūsuf alikuwa nyumbani kwake, alimtaka Yūsuf kwa upole na kubembeleza, kwa kuwa alimpenda sana na kwa ajili ya uzuri wake, na akamfungia milango na akasema kumwambia Yūsuf, «Njoo kwangu.» Akasema, «Najilinda kwa Mwenyezi Mungu na najihifadhi Kwake na kujihami kutokana na hayo unayoniitia ya kumfanyia hiana bwanangu aliyeyafanya mazuri mashukio yangu na akanikirimu. Sitamhini kwa watu wake. Hakika hafaulu anayedhulumu na akafanya mambo ambayo hatakiwi kuyafanya |