Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 54 - يُوسُف - Page - Juz 13
﴿وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ ٱئۡتُونِي بِهِۦٓ أَسۡتَخۡلِصۡهُ لِنَفۡسِيۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُۥ قَالَ إِنَّكَ ٱلۡيَوۡمَ لَدَيۡنَا مَكِينٌ أَمِينٞ ﴾
[يُوسُف: 54]
﴿وقال الملك ائتوني به أستخلصه لنفسي فلما كلمه قال إنك اليوم لدينا﴾ [يُوسُف: 54]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mfalme, mtawala wa Misri, ilipomfikia habari kwamba Yūsuf hana hatia, alisema, «Mleteni kwangu nipate kumfanya ni miongoni mwa marafiki wangu wa kikweli na washauri wangu.» Yūsuf alipokuja, na mfalme akasema na yeye, akajua kwamba yeye hana hatia na kwamba ni muaminifu sana na ni mwenye tabia njema, alimwambia, «Wewe leo hapa kwetu una heshima kubwa na unaaminiwa kwa kila kitu.» |