Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 2 - الرَّعد - Page - Juz 13
﴿ٱللَّهُ ٱلَّذِي رَفَعَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ بِغَيۡرِ عَمَدٖ تَرَوۡنَهَاۖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلّٞ يَجۡرِي لِأَجَلٖ مُّسَمّٗىۚ يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَ يُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُم بِلِقَآءِ رَبِّكُمۡ تُوقِنُونَ ﴾
[الرَّعد: 2]
﴿الله الذي رفع السموات بغير عمد ترونها ثم استوى على العرش وسخر﴾ [الرَّعد: 2]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ndiye Aliyeziinua mbingu saba kwa uweza Wake bila ya nguzo, kama vile ambavyo mnaziona, kisha akalingana - yaani akawa juu - ya Arshi kulingana kunakonasibiana na utukufu Wake na ukubwa Wake, na Akalidhalilisha jua na mwezi kwa manufaa ya waja, kila moja wapo ya viwili hivyo kinazunguka kwenye anga lake mpaka Siku ya Kiyama. Anapekesha, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, mambo ya ulimwenguni na Akhera, Anawafafanulia dalili zenye kuonyesha uweza Wake na kwamba yeye hakuna mungu isipokuwa Yeye, ili muwe na Imani ya kikweli kwa Mwenyezi Mungu na mjiyakinishe kurudi Kwake, mpate kuamini ahadi Yake ya thawabu na adhabu na mumtakasiye ibada Peke Yake |