Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 36 - الرَّعد - Page - Juz 13
﴿وَٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَفۡرَحُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَۖ وَمِنَ ٱلۡأَحۡزَابِ مَن يُنكِرُ بَعۡضَهُۥۚ قُلۡ إِنَّمَآ أُمِرۡتُ أَنۡ أَعۡبُدَ ٱللَّهَ وَلَآ أُشۡرِكَ بِهِۦٓۚ إِلَيۡهِ أَدۡعُواْ وَإِلَيۡهِ مَـَٔابِ ﴾
[الرَّعد: 36]
﴿والذين آتيناهم الكتاب يفرحون بما أنـزل إليك ومن الأحزاب من ينكر بعضه﴾ [الرَّعد: 36]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wale ambao tuliwapa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, yoyote kati yao mwenye kukuamini, kama 'Abdullāh bin Salām na Najashi, wanaifurahia Qur’ani uliyoteremshiwa kwa kuwa inaenda sambamba na kile walichonacho. Na miongoni mwa wale wanaojiweka pamoja kukupinga, kama Sayyid na 'Aqib: maaskofu wawili wa Najran , na Ka'b bin al-Ashraf, wanaokanusha baadhi ya yale uliyoteremshiwa. Waambie, «Mwenyezi Mungu Ameniamrisha nimuabudu Yeye Peke Yake na nisimshirikishe chochote. Nawaita watu wamuabudu, na Kwake Peke Yake ndio marejeo yangu na marudio |