Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 108 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ وَسَمۡعِهِمۡ وَأَبۡصَٰرِهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡغَٰفِلُونَ ﴾
[النَّحل: 108]
﴿أولئك الذين طبع الله على قلوبهم وسمعهم وأبصارهم وأولئك هم الغافلون﴾ [النَّحل: 108]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu Amewapiga muhuri nyoyo zao kwa ukafiri na ufadhilishaji dunia juu ya Akhera, hazitafikiwa na nuru ya uongofu, na Amewafanya viziwi masikio yao kutozisikia aya za Mwenyezi Mungu , kusikia kwa kuzingatia, na Amewafanya vipofu macho yao wasizione hoja zinazojulisha uungu wa Mwenyezi Mungu , na hao ndio wenye kughafilika na ile adhabu Aliyowaandalia Mwenyezi Mungu |