Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 127 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَٱصۡبِرۡ وَمَا صَبۡرُكَ إِلَّا بِٱللَّهِۚ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَلَا تَكُ فِي ضَيۡقٖ مِّمَّا يَمۡكُرُونَ ﴾
[النَّحل: 127]
﴿واصبر وما صبرك إلا بالله ولا تحزن عليهم ولا تك في ضيق﴾ [النَّحل: 127]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na vumilia, ewe Mtume, kwa maudhi yanayokupata katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka ikujie faraji, na hakukuwa huku kuvumilia kwako isipokuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani Yeye Ndiye mwenye kukusaidia na kukupa uthabiti, na usisikitike juu ya wale wanaoenda kinyume na wewe na wasiitikie ulinganizi wako, wala usiwe na usijitie dhiki za moyo kutokana na hila zao na vitimbi vyao, kwani hilo litawarudia wao wenyewe kwa shari na mateso |