Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 30 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿۞ وَقِيلَ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ مَاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمۡۚ قَالُواْ خَيۡرٗاۗ لِّلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٞۚ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞۚ وَلَنِعۡمَ دَارُ ٱلۡمُتَّقِينَ ﴾
[النَّحل: 30]
﴿وقيل للذين اتقوا ماذا أنـزل ربكم قالوا خيرا للذين أحسنوا في هذه﴾ [النَّحل: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wanapoambiwa Waumini wenye kumuogopa Mwenyezi Mungu, «Ni kitu gani Alichokiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Nabii Muhammad, rehema na amani zimshukie?» wanasema, «Mwenyezi Mungu Amemteremshia wema na uongofu.» Wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hapa duniani na wakawalingania waja wa Mwenyezi Mungu kwenye Imani na matendo mema, watapata heshima kubwa ya kupewa ushindi duniani na riziki kunjufu. Na nyumba ya Akhere ni bora kwao na ni kubwa kuliko vile walivyopewa duniani. Na nyumba yenye neema zaidi ya wale wachamungu wenye kumuogopa Mwenyezi Mungu ni Akhera |