Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 35 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَقَالَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ لَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا عَبَدۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖ نَّحۡنُ وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ فَهَلۡ عَلَى ٱلرُّسُلِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ ﴾
[النَّحل: 35]
﴿وقال الذين أشركوا لو شاء الله ما عبدنا من دونه من شيء﴾ [النَّحل: 35]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na washirikina walisema, «Lau kama Mwenyezi Mungu Alitaka tumuabudu Yeye Peke Yake, hatungalimuabudu yoyote asiyekuwa Yeye, sisi wala baba zetu kabla yetu, wala hatungaliharamisha chochote Asichokiharamisha». Ni hoja kama hizi za kipotofu walizozitumia makafifiri waliopita. Na wao ni warongo, kwani Mwenyezi Mungu Aliwaamrisha na Akawakataza na Akawawezesha kuyasimamia Aliyowakalifisha nayo, na Akawapa nguvu na matakwa yanayotokamana na vitendo vyao. Kwa hivyo, kujenga hoja kwao wakitegemea mapitisho ya Mwenyezi Mungu na makadirio Yake ni ubatilifu mkubwa baada ya kuonywa kwao na Mitume. Na Mitume wenye kuwaonya hawana la zaidi isipokuwa kuufikisha ujumbe ulio wazi waliokalifishwa nao |