Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 56 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَيَجۡعَلُونَ لِمَا لَا يَعۡلَمُونَ نَصِيبٗا مِّمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡۗ تَٱللَّهِ لَتُسۡـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمۡ تَفۡتَرُونَ ﴾
[النَّحل: 56]
﴿ويجعلون لما لا يعلمون نصيبا مما رزقناهم تالله لتسألن عما كنتم تفترون﴾ [النَّحل: 56]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa uovu wa matendo yao ni kwamba wao wanawatengea masanamu waliowafanya ni waungu, wasiojua chochote na wasionufaisha wala kudhuru, sehemu ya mali zao walizoruzukiwa na Mwenyezi Mungu ili kujisongeza kwao. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu! Mtaulizwa tena mtaulizwa Siku ya Kiyama kuhusu yale ya urongo ambayo mlikuwa mkimzulia Mwenyezi mungu |