Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 64 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِي ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ ﴾
[النَّحل: 64]
﴿وما أنـزلنا عليك الكتاب إلا لتبين لهم الذي اختلفوا فيه وهدى ورحمة﴾ [النَّحل: 64]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hatukukuteremshia Qur’ani, ewe Mtume, isipokuwa ni uwafunulie watu wazi yale ambayo walikuwa wakitafautiana juu yake, ya dini na hukumu, ili hoja zisimame kwao kwa maelezo yako ambayo hayauachii upotofu njia ya kuingia nyoyoni. Na kwa kuwa Qur’ani ni uongofu, haitoi nafasi ya kutunduwaa, nayo ni rehema kwa Waumini katika kufuata kwao uongofu na kujiepusha kwao na upotevu |