Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 63 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿تَٱللَّهِ لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٖ مِّن قَبۡلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ ٱلۡيَوۡمَ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ ﴾
[النَّحل: 63]
﴿تالله لقد أرسلنا إلى أمم من قبلك فزين لهم الشيطان أعمالهم فهو﴾ [النَّحل: 63]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Naapa kwa Mwenyezi Mungu, hakika tumewapeleka Mitume kwa makundi ya watu kabla yako, ewe Mtume, Shetani akawapambia matendo waliyoyafanya ya ukafiri, ukanushaji na kuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Yeye anasimamia kazi ya kuwapoteza wao ulimwenguuni, na hao wenye kupotezwa, watakuwa na adhabu kali yenye kuumiza kesho akhera |