Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 11 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿وَيَدۡعُ ٱلۡإِنسَٰنُ بِٱلشَّرِّ دُعَآءَهُۥ بِٱلۡخَيۡرِۖ وَكَانَ ٱلۡإِنسَٰنُ عَجُولٗا ﴾
[الإسرَاء: 11]
﴿ويدع الإنسان بالشر دعاءه بالخير وكان الإنسان عجولا﴾ [الإسرَاء: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na binadamu wakati mwingine hujiapiza mabaya nafsi yake au mtoto wake au mali yake awapo na hasira kama vile anavyoomba mema. Hii ni kwa sababu ya ujinga wa mwanadamu na pupa lake. Na miongoni mwa rehema ya Mwenyezi Mungu kwake ni kwamba Yeye Anayakubali maombi yake mema na sio mabaya na kwamba Yeye anajua kuwa yeye hakukusudia kutaka hilo. Hakika binadamu ana tabia ya kuwa na pupa sana |