Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 110 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿قُلِ ٱدۡعُواْ ٱللَّهَ أَوِ ٱدۡعُواْ ٱلرَّحۡمَٰنَۖ أَيّٗا مَّا تَدۡعُواْ فَلَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَلَا تَجۡهَرۡ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتۡ بِهَا وَٱبۡتَغِ بَيۡنَ ذَٰلِكَ سَبِيلٗا ﴾
[الإسرَاء: 110]
﴿قل ادعوا الله أو ادعوا الرحمن أيا ما تدعوا فله الأسماء الحسنى﴾ [الإسرَاء: 110]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina wa watu wako waliokupinga kutumia kwako neno la Yā Allāh , Yā Raḥmān, katika maombi, «Muombeni Allāh (Mwenyezi Mungu) au muombeni Raḥmān (Mwingi wa rehema), kwani kwa majina yoyote yake mkimuomba huwa mnamuomba Mola Mmoja, kwa kuwa majina Yake yote ni mazuri. Wala usidhihirishe kisomo katika Swala yako wakakusikia washirikina, wala usisome kwa siri wasikusikie masahaba zako, na uwe kati na kati baina ya kudhihirisha na kusirisha.» |