×

Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na wakusanyie jeshi lako 17:64 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Isra’ ⮕ (17:64) ayat 64 in Swahili

17:64 Surah Al-Isra’ ayat 64 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 64 - الإسرَاء - Page - Juz 15

﴿وَٱسۡتَفۡزِزۡ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتَ مِنۡهُم بِصَوۡتِكَ وَأَجۡلِبۡ عَلَيۡهِم بِخَيۡلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكۡهُمۡ فِي ٱلۡأَمۡوَٰلِ وَٱلۡأَوۡلَٰدِ وَعِدۡهُمۡۚ وَمَا يَعِدُهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ إِلَّا غُرُورًا ﴾
[الإسرَاء: 64]

Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali na wana, na waahidi. Na Shet'ani hawapi ahadi ila ya udanganyifu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: واستفزز من استطعت منهم بصوتك وأجلب عليهم بخيلك ورجلك وشاركهم في الأموال, باللغة السواحيلية

﴿واستفزز من استطعت منهم بصوتك وأجلب عليهم بخيلك ورجلك وشاركهم في الأموال﴾ [الإسرَاء: 64]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
«Na uwalaghai wale unaoweza kuwalaghai miongoni mwao kwa kuwaita kuniasi, na uwakusanyie askari zako unaowaweza, kati ya kila aliye juu ya kipando na anayetembea kwa miguu, na ujishirikishe nao katika mali yao wanayoyachuma kwa njia za haramu, na ujishirikishe nao katika watoto wao kwa kuwapambia uzinifu na uasi na kwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu mpaka uenee uchafu na uharibifu, na uwaahidi wafuasi wako, miongoni mwa wale wanaozalikana na Ādam, ahadi za urongo, na kila ahadi za Shetani ni ubatilifu na udanganyifu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek